Saturday 23 February 2013

Siri ya Mtungi



Siri ya Mtungi Sehemu ya 1


Jina: Siri ya Mtungi


Aina ya Mchezo: Tamthilia yenye Kuendelea

Mtayarishaji:John Ribber

Mwongozaji wa filamu (Director) Jordan Ribber, Tito Mwaipopo, Modesta Kuzenzia,

Lugha: Kiswahili (Tafasiri ya Kiingereza na Ali Mbwana)

Watayarishaji: ‘Siri ya Mtungi’ imetayarishwa na MFDI Tanzania ikishirikiana na JHUCCP Tanzania kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia USAID.

Mwendelezo: Andrew Whaley, Ali Mbwana na Carola Kinasha

Umri: Filam ya Kifamilia


Wahusika wa Mchezo:

•             Juma Rajab: .......................................Cheche Mtungi <<link>>
•             Godliver Gordian: .............................Cheusi Mtungi <<link >> 
•             Suleiman Mambo Suleiman: .............Shoti <<link>>
•             Patrick John Masele: ..........................Dafu <<link>>
•             Steven: ...............................................Yaeli Aloyce Kazimbaya <<link>>
•             Daudu Michael: .................................. Duma <<link>>
•             Hidaya Maeda:  .................................... Nusura <<link>>
•             Nkwabi Elias Ng'hangasama: ................. Mzee Kizito <<link>>
•             Betty Aloyce Kazimbaya: ....................... Mwanaidi  <<link>>
•             Halima Maulid: ...................................... Farida <<link>>
•             Yvonne Cherrie:               ..................................... Lulu <<link>>
•             Beatrice Taisama: .................................. Tula <<link>>
•             Patricia Edward Nyamaka: ..................... Sabrina <<link>>
•             Mac-Donald Martin Haule: ..................... Masharubu <<link>>
•             Khalid Jumanne Nyanza: ........................  Kovu <<link>>

Wadhamini:
Media for Development International, Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (JHU•CCP) na USAID

Kwa Ufupi (Storyline|Plot): Maelezo Ya Jumla Ya Hadithi - Siri Ya Mtungi

“Siri ya Mtungi” ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha, inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu. Cheche anampenda sana mkewe, lakini mawazo ya kuanzisha biashara mpya na kuwepo ujio wa mtoto mwingine wa tatu yanawapa wakati mgumu. Anajaribu kuwa baba mwema, lakini, kama ni uchawi au bahati tu, anawavutia sana wanawake…na wale makahaba! Cheche pia ana uhusiano wa karibu na mpenzi wake wa shuleni, Tula.

Kizito, ni baba mkwe wake Cheche, aliyemsaidia kuanzisha biashara yake. Ni mtu anayeheshimika sana katika jamii ya Bagamoyo na kila mara anashughulika na watoto wake Nuru na Matona katika karakana yake ya magari. Pamoja na hayo, Kizito ana watoto wengine wengi aliozaa na wake zake watatu, Farida, Mwanaidi na Vingawaje, aliyefariki hivi karibuni.

Mhalifu wa mjini ni Masharubu, tajiri mwenye nguvu anayemiliki mabanda na biashara za kitapeli. Baada ya kuvumilia matusi kwa muda mrefu, mkewe alimkimbia na kumwachia binti yao mrembo, Nusura. Nusura ni ua la yungiyungi lililochanua kwenye lile gheto. Ni mjanja, mwanamke shupavu ambaye udhaifu wake ni mahusiano yake na Duma, mmoja wa wapangaji wa Masharubu. Duma ana moyo wa dhahabu lakini anahangaika kimaisha kama DJ mjini Bagamoyo.Karibuni tu alimleta mdogo wake, Stephen, toka kijijini, ili mvulana huyo aingie shule ya kujitegemea na kupata fursa ya maisha bora lakini, mpaka muda huu Duma anashindwa kumtimizia mahitaji muhimu. Muhimu zaidi, Duma anashindwa kuwa mfano bora kwa mdogo wake, Stephen anayechoshwa na shule na kutaka kuwa ‘mtoto wa mjini’ kama kaka yake.

Nyendo za Nusura na Kizito zinapishana kuashiria bahati kwa Kizito, ambaye yuko tayari kuendelea mbele na maisha yake kufuatia kifo cha mkewe mdogo. Nusura kwa upande wake amechoshwa na wasiwasi katika mahusiano yake na Duma, hivyo yuko tayari kwa mambo ya kiungwana zaidi. Nusura anajikuta yuko njia panda kati ya penzi la Duma na lile lililotulia kama maji lenye uelekeo wa ndoa na Kizito. Hana ufahamu wowote kuwa kuna dhoruba inayochemka katika maji yale ya samawati. Siri zitasimuliwa, maisha kuchanwachanwa na mioyo kuvunjwa kwenye mji huu wa Bagamoyo.


Mapitio: (Review)
Tamthilia ya Siri ya Mtungi ni nzuri inayofaa kutazamwa na familia nzima, japokuwa kuna vipande vichache ambavyo si vizuri sana kwa watoto, Tamthilia hii imepangwa vema na mtiririko wenye kueleweka japokuwa nayo ina matatizo kidogo haswa kwa baadhi ya Waigizaji kuongea kama wamekariri, mfano hai ni Mzee Kizito, Stephen na baadhi ya waigizaji...!

Pongezi kubwa kwa Tamthilia hii, haswa kwa maamuzi yao ya kutumia mazingira halisi ya Mtanzania wa kawaida na wahusika kuvaa uhalisia...! Muziki  wa ala upo kwenye maadhi ya Kitanzania na nyimbo ni za Kitanzania kwa asiliamia kubwa. Kwa kweli wamejitahidi sana,ukilinganisha na watayarishaji wengine wa Bongo movies, labda kwa kuwa wanapata surpot na wataalam kutoka Marekani, na watayarishaji wenye uzoefu wa muda mrefu.
Kuanzishwa kwa tamthilia hii, inaweza kuwa chachu kwa watayarishaji wengine kuiga yale mazuri, na haswa aina ya upigaji picha, mazingira na matumizi ya rasilimali za Kitanzania.
Angalia mtitiriko mzima wa tamthilia hii hapa: <<link>>

No comments:

Post a Comment