Saturday 2 March 2013

Lafudhi Isiwe Kizuizi


Mwandishi: Idd Ninga

Lafudhi Isiwe Kizuizi Cha Filamu Ya Msanii Mchanga Kutosambazwa

Ni wakwti mwingine tena ambao tunakutana pamoja tukiwa wazima na afya tele,na huo siyo uwezo wetu bali ni mapenzi ya yule alotuleta katika dunia hii.

Lafudhi ni jambo la kawaida kwa kila mtu,kila jamii,kila taifa na kila tabia,na takribami dunia nzima kila jamii au taifa kwa ujumla huwa na lafudhi zao.

Leo ningelipenda kutazama upande wa lafudhi za kitanzania,nchi ambayo imejaaliwa kuwa na makabila mengi na takribani makabila yote kila moja lina lafudhi yake,hali hiyo inaifanya nchi yetu kuwa yakipekee duniani kutokana na wananchi wake kuwa na lafudhi tofauti tofauti japokuwa woote tunazungumza kiswahili na kuelewana vyema. Tasnia ya filamu katika nchi yetu inakuwa kwa kasi sana, hali inayofanya makampuni mengi ya utengenezaji na usambazaji wa filamu kuanzishwa na takribani kila siku makundi mapya kutoka sehemu
mbalimbali za nchi ya tanzania huanzishwa kwa malengo ya kutengeneza filamu.

Wasanii wengi hasa wachanga (up coming)wamekuwa katika changamoto kubwa ya lafudhi,hali ambayo inafanya filamu zao nyingi kugomewa na wasambazaji kwa kigezocha lafudhi.
Lafudhi zilizopo katika filamu zetu ndio uhalisia halisi wa mtanzani na wala siyo jambo la kuigiza. Jambo la ajabu na la kushangaza ni pale unapopeleka filamu yako kwa
msambazaji na kuambiwa kuwa filamu yako haifai kwa kigezo cha lafudhi,swali la kujiuliza ni kwamba hawa wasambazaji wanasiri gani ya kususia filamu zetu kwa kigezo cha lafudhi na hali kuwa sisi tunaona filamu kutoka nje zikiingia katika soko la dunia huku zikiwa na lafudhi zao husika,nchi kama Nigeria inasambaza film zake huku wakitumia lafudhi yao na filamu zimakubalika katika soko,sasa iweje kwa mtanzania kugomewa film kama siyo kuonyesha kwamba lul,gha ya Tanzani na lafudhi yake siyo chochote siyo lolote,kwa maoni yangu huu ni ubaguzi tene ubaguzi wa wazi ambao unatakiwa kupigwa vit kwa hali yoyote ile.

Msambazaji anakiri kuwa filamu imetengenezwa vizuri kuanzia katika story, scipt, hisia, shot na uhalisia lakina unakosolewa kuwa lafudhi yako ni mbaya eti inafanana na kiarusha au kimasai au kisukuma au kichaga. Jambo hili linatia hasira hasa pale unapokutana na mtu ambae hta hana asili ya kitanzania akikwambia maneno kama hayo.
Jambo hili lilishafika hata kwa ndugu Simoni Mwakifamba na mpaka sasa hatujapata taarifa rasmi kuhusu suluhisho la hilo huku wasanii wa kanda kama ya kaskazini wakiwa waathirika wakubwa wa jambo hilo.

Tunaiomba serikali iliyazame hili kwa jicho la haki na kuona kuwa wananchi wake wanafanyiwa unyanyasaji na wasambazaji wa filamu kwa kigezo cha lafudhi,kwa hili naweza kusema kuwa LAFUDHI NI ASILI YA MUAFRIKA NA MATANZANI anaechukia lafudhi hiyo bora ahame nchi.

Filamu na kiwanda kikubwa cha kuzalisha ajira kwa mtanzani,hivyo ni jukumu la serikali kulisimamia hili,kwani iwapo tutaacha lafudhi zetu na kuiga lafudhi nyingine tutaku hatupo katika uhalisia na uhalisia ni jambo la muhimu katika uundaji wa filamu yenye ubora

No comments:

Post a Comment