About us


Blog ya Bongo Film Review & Critics, itakuwa ikiruhusu watu watume kwenye blog aina mbalimbali za filamu zinazotengenezwa Bongo, dhumuni haswa ni Kukosoa, Kusifia na kufanya uchambuzi na kuzitathmini filamu za hapa nyumbani.

Kazi hii haitafanywa na Administrators wa Bongo Film Review & Critics Hapana, ila kwa kila mwenye nafasi ya kufanya hivyo anaruhusiwa kutuma maoni yake moja kwa moja kwa kupitia email hii: bongofilmreview@gmail.com Nasi tutayaweka hewani moja kwa moja.

Itapendeza sana watumaji na watoa maoni wakazingatia mambo kadhaa, yakiwemo:


  • Kuweka kwa ufupi Simulizi ya Mchezo husika (Storyline| Plot)
  • ·        Aina ya Mchezo wenyewe: (Genre) Action | Adventure | Crime | Thriller | Love Story |
  • ·        Umri wanaopaswa kuangalia huo mchezo.
  • ·        Waigizaji (Actors & Actress) | Wahusika wa Mchezo
  • ·        Mtunzi wa huo mchezo:
  • ·        Mwongozaji wa filamu (Director)
  • Baada ya hapo unaweza ukaandika chochote kile kuhusiana na huo mchezo kwa kuangalia Makosa kwenye filamu.
  • ·        Lugha zinazotumika,  Makosa kwenye Tafasiri, (Kiswahili kwenda Kiingereza)
  • ·        Upigaji au uchukuliwaji wa picha na sehemu zilizotumika kama zinaendana na simulizi. Hali halisi ya kimazingira na filamu yenyewe... Mazingira ya Uigizaji kama yanaendana na hali halisi.
  • ·        Matumizi ya sound effect na background sound. Je zimetumika sauti na mziki na nyimbo za Kiswahili au wa nje ya nchi, kwanini.

Mahoni yako kwa ujumla, na huo mchezo unatoa Nyota ta ngapi...

Nyota 1 – Haifai, ni kupoteza pesa kuiangalia
Nyota 2 – Waweza kuangalia, lakini hafurahishi
Nyota 3  – Inafaa
Nyota 4  – Nzuri na inavutia
Nyota 5  – Nzuri na unashauri watazamaji waitafute ili waiangalie.

Karibuni sana.





No comments:

Post a Comment