Na
Iddy A. Ninga
Katika
hali isiyo ya kawaida lile kundi kongwe la sanaa za filamu mkoani Arusha ambalo
bado halijafanikiwa kutokelezea na kuweka mizizi yake ndani ya Tanzania
limejikuta likipata saluti ya heshima kutoka kwa katibu wa TDFF mkoa wa Arusha
ajulikanae kwa jina la Kimu.
Saluti hiyo ya heshima
ilikuja mara baada ya katibu huyo kuona kazi kubwa inayoendelea ndani ya kundi
hilo. Uongozi wa chama cha wasanii mkoa wa Arusha upo katika harakati za
kutembelea makundi mbalimbali ya filamu mkoani hapa kwa lengo la kuhamasisha
umoja na ushirikiano kwa wasanii wa Arusha na Tanzania.
Wasanii wengi wa mkoa wa
Arusha wapo katika harakati za kuungana na kujiweka katika umoja mzuri ambako
mpaka sasa kundi la Agesta liliweza kuaanda onyesho maalumu lililoitwa
pamoja party ambalo walikuwa na lengo la
kuwakutanisha wasanii wote wa Arusha lakini maajabu ya musa ni kundi moja tu la
cultural group ndilo liloonyesha ushirikiano katika tukio hilo na makundi yote
yalibaki nyuma bila ya kuonyesha ushirikiano unaotakia hali ambayo inaonyesha
kuwa bado ushirikiano ni mdogo ndani ya mkoa huu.
Katibu wa TDFF alisema kuwa
bado wapo katika harakati kubwa za kupigania haki za wasanii mkoani Arusha na
chama kama chama kinafikiria kupanga bei ya shilingi elfu mbili kwa copy moja
ili msanii apatea faida na siyo msambazaji peke yake.
Hadi sasa wasanii wa mkoa wa
Arusha bado wanadai kuwa COSOTA haifanyi kazi kwa faida ya wasanii bali infanya
kazi kwa manufaa ya msambazaji peke yake.
Wasanii wengi wanadai kuwa
afisa utamaduni wa wilaya ya Arusha hafanyi kazi pamoja na wasanii wa mkoa huu
hali inayofanya wasanii hao kudai uhalali wa afisa huyo.
Agesta Sanaa Group ni kundi
maarufu ndani ya mkoa wa Arusha na katibu wa TDFF alishangazwa baada ya kuona
kazi nzuri inayofanyika ndani ya kundi hilo licha ya maneno ya uzushi yanayosemwa
kuwa Agesta imekufa.
Wasanii wa Arusha bado wapo
katika harakti za kujikomboa ili wafaidike na kazi wanazo fanya.
No comments:
Post a Comment