Saturday 4 May 2013

Tamthilia ya Pembe Nne: Mabadiliko Yaanza Kuonekana

Na Iddy A. Ninga

Mabadiliko yanaanza kuonekana katika Tasnia ya sanaa za filamu Tanzania.

Kwa muda mrefu wa kazi wa Arusha walikuwa katika kilio kizito dhidi ya wasambazaji wa filamu Tanzania ambao walikuwa wakilalamikiwa kwa kugomea filamu kwa kisingizio cha lafudhi, lakini sasa kwa mara ya kwanza tamthili ijulikanayo kwa jina la PEMBE NNE imeonyeshwa kwa kipindi cha miezi kadhaa na kuonyesha matumaini makubwa kwa wasanii watokao kanda ya kaskazini.
Ikiwa ni tamthili ya kwanza kutoka Arusha kuonyeshwa katika kituo kikubwa cha television licha ya kuwa kuna tamthilia kadhaa ziliwa kuandaliwa na wasanii wa Arusha na hata kuonyeshwa kwa majaribio na kutokea kupendwa na watazamaji wengi.

Moja kati ya tamthilia iliyowahi kutayarishwa ndani ya jiji la arusha ni ile ya HAIBA YA PENZI ambayo haikufanikiwa kumalizika kutokana na matatizo ya kugawanyika yalotokea ndani ya kundi la AGESTA na kusababisha tamthilia hiyo kuishia hewani.

CHIGANGA ni kundi ambalo linaelekea kupata umaarufu mkubwa katika tasnia ya filamu mkoani Arusha na Tanzania kutokana na tamthilia yao ya PEMBE NNE kuendelea kushika kasi katika kituo kimoja cha television hapa nchini.

Katika tamthilia hiyo mambo kadhaa yameeonyeshwa na kufanya tamthilia kwa kiwango fulani kuvutia. Ndani ya tamthilia hiyo pameonyeshwa msomi wa hali ya juu akiwa ni mtu wa kwanza kuwatenga watu wenye ulemavu na kuwafungia ndani ili wasijulikane lakini mwisho wanafunzi wa shule wanaamua kufichua siri hiyo na kumtoa mlemavu huyo na jamii inagundua siri nzito katika familia hiyo.

Jambo jingine lenye kuvutia zaidi ndani ya tamthilia ya pembe nne ni kitendo cha mlemavu wa miguu kuonyesha kuwa anauwezo wa kufanya kazi kubwa na nzuri zaidi ya hata yule mwenye kuwa na viungo kamili. Alionekana mzee mmoja mwenye ulemavu akiwa ni daktaria, hali hiyo inafanya kuwa walemavu wanaweza iwapo watapewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao.
Tamthilia ya PEMBE NNE haikuwa mbali sana kuonyesha matatizo na changamoto zilizoko mashuleni na mitaani hali ambayo inawafanya vijana wengi kuwa katika wakati mgumu kukamilisha ndoto zao.

Ni tamthilia ambayo kwa kiasi kikubwa inavutia na kupendeza ndani ya macho ya mtazamaji ukiachilia mbali matatizo madogo madogo yaliyopo ndani yake.
Mimi kwa tathimini yangu kuna watu kadhaa ambao ningependa kuwapa sifa kutokana na uwezo wao mzuri walouonyesha ndani ya tamthilia hiyo.

Mtu wa kwanza ni aliye igiza  kama taira na kufungiwa ndani, kwa asilimia kubwa kaonyesha uwezo wa hali ya juu hasa kutokana na nafasi alopewa, mtu mwingine ambae alionyesha uwezo mkubwa ni mwanamke aliye igiza kama matron wa shule (Habari tulizo nazo, ni kwamba mwigizaji huyo amefariki dunia) ameonyesha maajabu pale alipokuwa akitokwa machozi kutokana na makosa wanayofanya wanafunzi wawapo shuleni, alionekana kuwa ni mwalimu alietaka wanafunzi wake wawe katika mstari mzuri bila ya kutumia adhabu kali.

Jambo jingine ambalo ni la muhimu kujua ni kwamba neno PEMBE NNE linamaanisha nini katika mchezo huo? Nadhani lina maanisha Maisha kwa Ujumla wake.

No comments:

Post a Comment