Thursday 30 May 2013

Agesta Yazidi Kutamba Mkoani Arusha.

 Mwenyeketi Aipigia Saluti.

Na Iddy A. Ninga

Katika hali isiyo ya kawaida lile kundi kongwe la sanaa za filamu mkoani Arusha ambalo bado halijafanikiwa kutokelezea na kuweka mizizi yake ndani ya Tanzania limejikuta likipata saluti ya heshima kutoka kwa katibu wa TDFF mkoa wa Arusha ajulikanae kwa jina la Kimu.

Saluti hiyo ya heshima ilikuja mara baada ya katibu huyo kuona kazi kubwa inayoendelea ndani ya kundi hilo. Uongozi wa chama cha wasanii mkoa wa Arusha upo katika harakati za kutembelea makundi mbalimbali ya filamu mkoani hapa kwa lengo la kuhamasisha umoja na ushirikiano kwa wasanii wa Arusha na Tanzania.

Wasanii wengi wa mkoa wa Arusha wapo katika harakati za kuungana na kujiweka katika umoja mzuri ambako mpaka sasa kundi la Agesta liliweza kuaanda onyesho maalumu lililoitwa pamoja  party ambalo walikuwa na lengo la kuwakutanisha wasanii wote wa Arusha lakini maajabu ya musa ni kundi moja tu la cultural group ndilo liloonyesha ushirikiano katika tukio hilo na makundi yote yalibaki nyuma bila ya kuonyesha ushirikiano unaotakia hali ambayo inaonyesha kuwa bado ushirikiano ni mdogo ndani ya mkoa huu.
Katibu wa TDFF alisema kuwa bado wapo katika harakati kubwa za kupigania haki za wasanii mkoani Arusha na chama kama chama kinafikiria kupanga bei ya shilingi elfu mbili kwa copy moja ili msanii apatea faida na siyo msambazaji peke yake.

Hadi sasa wasanii wa mkoa wa Arusha bado wanadai kuwa COSOTA haifanyi kazi kwa faida ya wasanii bali infanya kazi kwa manufaa ya msambazaji peke yake.

Wasanii wengi wanadai kuwa afisa utamaduni wa wilaya ya Arusha hafanyi kazi pamoja na wasanii wa mkoa huu hali inayofanya wasanii hao kudai uhalali wa afisa huyo.
Agesta Sanaa Group ni kundi maarufu ndani ya mkoa wa Arusha na katibu wa TDFF alishangazwa baada ya kuona kazi nzuri inayofanyika ndani ya kundi hilo licha ya maneno ya uzushi yanayosemwa kuwa Agesta imekufa.

Wasanii wa Arusha bado wapo katika harakti za kujikomboa ili wafaidike na kazi wanazo fanya.

No comments:

Post a Comment