Saturday 8 June 2013

Sanaa Ya Arusha Yaanza Kuonyesha Mabadiliko.

·         Agesta yajipanga kutetea tasnia hiyo.
·         Food supply yamtetemesha katibu wa tdfaa.
·         Wengine waaswa kufata nyayo za Agesta.

Na Iddy A. Ninga

Lile kundi mahiri la sanaa za filamu mkoan Arusha lijulikano kwa jina la Arusha Group Educating Society Through Art maarufu kwa jina la Agesta limekuja na mbinu mpya na ya aina yake katika kuonyesha njia msanii kuwa anatakiwa kufanya kazi nyingine na siyo kutegemea maigizo ya filamu peke yake.

Kundi hilo ambalo siku chache zilizopita lilipata Saluti ya heshima kutoka kwa katibu wa Tadafa kutokana na mambo mazuri wanayoyafanya.

Hivi karibuni wameanzisha biashara mpya ya kusambaza vyakula maofisini mjini Arusha, kwa lengo la kujiongezea kipato. Biashara walio ianzisha wameipa jina la Agesta Food Supply.

Mmoja wa wadau katika harakati hizo za kujiongezea kipato kwa jina la Joseph Raphael (Batista) alisema kwamba wameamua kuanzisha biashara hiyo kwa lengo la kuionyesha jamii kuwa wao wapo kwa ajili ya jamii na kutoa elimu ndani
ya jamii ili kila mtu ajue kuwa msanii anatakiwa kuitumikia jamii
ipasavyo na siyo kutengeneza filamu kila siku na kusahau kuwa katika
jamii kuna mambo mengi ya kufanya na wao ndio kioo cha jamii na wengi
wanawatazama wao.

Kwa sasa Agesta wamenza rasmi kusambaza vyakula katika maofisi yaliyoko jijini Arusha na wakiwapa nafasi wateja wao kuagiza vyakula wanavyopenda na kuletewa kwa wakati.

Watu kadhaa walio bahatika kupata uduma hii ya kuletewa vyakula maofisini wameshauri pia vikundi vingine vya sanaa kuiga mfano wa Agesta ili waweze kujiongezea kipato na maendeleo katika soko la ajira.


Na Katibu wa chama cha wasanii mkoani Arusha, aliwapongeza wasanii wa
Agesta kwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na haswa kwa wakazi wa Arusha, kwa kuzingatia kuwa swala la ajira limekuwa ni tatizo la kitaifa na kwa ubunifu wao itakuwa ni chachu na  mwanzo wa kufika katika malengo walioyo jipangia.

No comments:

Post a Comment