Tuesday 9 April 2013

Arusha Movie Yanuka.


·         Milioni Kumi Zachakachuliwa.
·         Waandishi Wa Habari Wabebeshwa Lawama.
·         Viongozi Watakiwa Kuachia Madaraka.

Na Iddy A Ninga

Sakata kubwa limezuka ndani ya mkoa wa Arusha kufuatia wasanii wa filamu kuhoji juu ya uhalali wa viongozi waliopo madarakani kushikilia nyadhifa hizo.

Hayo yalizuka siku ya jana tarehe saba kufuati kikao kilichokaliwa na wasanii katika mkoa huo na kusababisha kuzuka kwa malumbano ambayo yalitaka kusababisha kikao hicho kuvunjika. Katika kikao hicho ambacho mwanzo kilianza kwa kutaja ajenda sita za kikao hicho na badala yake ikajadiliwa ajenda moja na kabla ya ajenda haijaisha yalizuka madai ya wasanii kuhoji juu ya uhalili wa viongozi wa shirikisho la mkoa ambao viongozi hao hao ndio viongozi wa Arusha movie.

Katika madai ya wasanii hao, walidai kuwa Arusha Movie imetumia shilingi milioni kumi zilizotolewa na NSSF na vingozi walipoulizwa kuhusu hilo walidai kuwa pesa hizo zilitolewa kwa ajili ya Arusha movie na wala siyo kwa ajili ya shirikisho la wasanii wa filamu mkoa wa Arusha.
Akijibu tuhuma hizo Bwana Kasimu Digega ambae ni mwenyekiti wa wasanii Arusha alisema kwamba wakati pesa hizo zikitolewa yeye alikuwa mjumbe wa Arusha movie na wala hakua kiongozi bali pesa hizo zilichukuliwa na viongozi wawili ambao ni Bwana Isack Chalo na Hussen Sichonge maarufu kwa jina la Ngwasuma.

Hussen Sichonge alikiri kuwa yeye ndie aliehusika na kuchukua pea hizo na pia alidai kuwa kuna watu wametumwa kuja kuharibu kikao kilichofanyika siku ya jana. Bwana Hussein Sichonge alianza kutoa lawama zake kwa mwanadada ajulikanae kwa jina la Neshika kuwa ni mmoja kati ya watu walo tumwa kuja kuharibu kikao hicho, pia msanii na mwandishi wa habari ajulikanae kwa jina la Severinus Mwijage alilaumiwa na bwana Sichonge kuwa na yeye katumwa na Mr Eliasi Magesa ili kuja kuharibu mkutano huo wa wasanii.

Wasanii hao waliwataka viongozi wa shirikisho kujiuzulu kufuatia vingozi hao kushikilia nyadhifa mbili tofauti na wasanii kuona kuwa maslahi yao yanapigwa panga na viongozi wao kwani linapokuja suala la pesa linabebwa na Arusha Movie na siyo shirikisho.

Wasanii hao waliendelea kudai kuwa muda wa viongo waliopo madarakani muda wao umeisha na hawatakiwa kufanya tena kazi za shirikisho kutokana na muda wao kuisha.

Pia bwana Kasimu Digega aliwalaumu waandishi wa habari wa Arusha kwa kutaka pesa ili kutoa habari za wasanii wa filamu. Hadi muda huu wasanii wa Arusha wanamsubiri kwa hamu raisi wa Taff Bwana Simon Mwakifamba ili kuja kutoa suluhisho la jambo hilo na asilimia kubwa ya wasanii wa Arusha wanaonekana kuukataa uongozi uliopo sasa na kutaka, uongozi mpya ambao utasimama kama shirikisho na siyo Arusha Movie ambao ni kikundi cha watu wachache.
Kufuatia sakata hilo NSSF wanawajibu wa kutoa kauli juu ya milioni kumi walizotoa na kufanya semina wasanii wa Arusha huku asilimia kubwa wakiwa wamejiunga na NSSF.

Hadi sasa bado wasanii wa Arusha hawapo katika muelekeo mzuri na bado hawaitambui tofauti ya Arusha Movie na shirikisho.


No comments:

Post a Comment