Thursday 4 April 2013

The Lost Adam




·        Story:  Mtitu G. Game
·        Script: Ali M. Yakuti
·        Make-up & Continuity: Mayasa Mrisho,
·        Camera: Leonard Muhumbira
·        Sound: Rahim Khatibu
·        Editor: Leornard Muhumbira
·        Music: Beny Chaila
·        Mastering: Mtitu G. Game
·        Production Manager: Mayasa Mrisho
·        Assistant Producer: Mayasa Mrisho
·        Executive Producer: Mtitu G Game
·        Director: Mtitu G Game
·        Cast: Jacob Stephen, Rose Ndauka, Hemed Suleiman, Warda Walid, Patcho Mwamba

Ø Mchambuzi: Iddy A Ninga

The Lost Adam ni moja kati ya filamu ambayo ningependa kuizungumzia kwa siku ya leo.
Nianzie na upande wa umri, kwa kifupi filamu hiyo ilikuwa inatakiwa kutazamwa na watu wa kuanzia umri wa miaka kumi na nane kutokana na kipande ambacho kinamuonyesha Adamu na Tamara wakiwa wamelaliana juu ya kochi na hiyo ni baada ya mke wa adamu kuaga anakwenda safari.

Kutokana na kipande hicho kuwa ni nyeti zaidi na kinaweza kuleta madhara fulani kwa jamii hasa watoto wadogo ambao umri wao haulingani na kutazama matukio kama kulingana na umri wao.
Katika filamu nyingi za kitanzania, wachezaji wengi hasa wa upande wa ulinzi wamekuwa na mtindo wa kucheza watu wa vituko kitu ambacho katika maisha ya uhalisia hakipo, na tumeona sasa hivi walinzi ni watu wa kawaida na heshima zao.

Katika filamu hii mlinzi alikuwa ni mtu wa vituko, jambo kama hili siyo lazima lionekana sana katika movie zetu kwani kuna uwezekano mkubwa wa kumtoa mtu katika maisha ya uhalisia.
Kwa upande wa rangi kuna sehemu rangi za chumba zilikuwa zikiingiliana, mfano tazama kipande ambacho mke wa adamu alipokea simu ya mume wake. Sauti nayo ilikuwa inasikika katika hali ambayo haikuwa vizuri sana ingawa ilikuwa ikisikika vizuri kabisa. Sauti ilikuwa ikisikika kama mtu yupo ndani na muda huo huo mtu anaonekana yupo nje.

Kwa upande wa ubunifu, filamu ilikuwa na ubunifu mwingi na kumfanya mtazamaji kujisikia raha hasa pale ilipogundulika kuwa mke wa Adanu hakufa ila alijichimbia mahali ili kilinda maisha yake. Pia ubunifu katika familia ya Adamu ulikuwa mzuri na kusikitisha sana, hasa pale unapotazama jinsi familia ilivokuwa katika hali fulani ya utofauti wa maisha.

Filamu ilikuwa nzuri sana ila kwa ushauri wangu, kama filamu ingekuwa na sehemu wa kwanza peke yake ingekuwa nzuri zaidi na ingekubalika na wengi kwani ukweli ni kwamba watanzania wengi wanachukia filamu yenye part one na kuendelea...

No comments:

Post a Comment