Siri ya Mtungi Sehemu ya 1
Jina: Siri ya Mtungi
Tovuti: http://www.siriyamtungi.com/
Aina ya Mchezo: Tamthilia yenye Kuendelea
Mtayarishaji:John Ribber
Mwongozaji wa filamu (Director) Jordan Ribber, Tito Mwaipopo, Modesta Kuzenzia,
Lugha: Kiswahili (Tafasiri ya Kiingereza na Ali Mbwana)
Watayarishaji: ‘Siri ya Mtungi’ imetayarishwa na MFDI Tanzania ikishirikiana na JHUCCP
Tanzania kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia USAID.
Mwendelezo: Andrew Whaley, Ali Mbwana na Carola Kinasha
Umri: Filam ya Kifamilia
• Juma
Rajab: .......................................Cheche Mtungi <<link>>
• Godliver
Gordian: .............................Cheusi Mtungi <<link >>
• Suleiman
Mambo Suleiman: .............Shoti <<link>>
• Patrick
John Masele: ..........................Dafu <<link>>
• Steven:
...............................................Yaeli Aloyce Kazimbaya <<link>>
• Daudu
Michael: .................................. Duma <<link>>
• Hidaya
Maeda: ....................................
Nusura <<link>>
• Nkwabi
Elias Ng'hangasama: ................. Mzee Kizito <<link>>
• Betty
Aloyce Kazimbaya: ....................... Mwanaidi <<link>>
• Halima
Maulid: ...................................... Farida <<link>>
• Yvonne
Cherrie:
..................................... Lulu <<link>>
• Beatrice
Taisama: .................................. Tula <<link>>
• Patricia
Edward Nyamaka: ..................... Sabrina <<link>>
• Mac-Donald
Martin Haule: ..................... Masharubu <<link>>
• Khalid
Jumanne Nyanza: ........................
Kovu <<link>>
Wadhamini:
Media for Development International, Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (JHU•CCP) na USAID
Media for Development International, Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health Center for Communication Programs (JHU•CCP) na USAID
Kwa Ufupi
(Storyline|Plot): Maelezo Ya Jumla Ya Hadithi - Siri Ya Mtungi
“Siri ya Mtungi” ni tamthilia ya televisheni inayofurahisha,
inayoonyesha maisha ya Cheche, mpigapicha mwenye bashasha na mmiliki wa Studio
ya Kupiga Picha ya Mtungi. Ana mke mrembo, Cheusi, aliyemzalia watoto wawili
wenye afya na huku akiwa na ujauzito wa mtoto wa tatu. Cheche anampenda sana
mkewe, lakini mawazo ya kuanzisha biashara mpya na kuwepo ujio wa mtoto
mwingine wa tatu yanawapa wakati mgumu. Anajaribu kuwa baba mwema, lakini, kama
ni uchawi au bahati tu, anawavutia sana wanawake…na wale makahaba! Cheche pia
ana uhusiano wa karibu na mpenzi wake wa shuleni, Tula.
Kizito, ni baba mkwe wake Cheche, aliyemsaidia kuanzisha
biashara yake. Ni mtu anayeheshimika sana katika jamii ya Bagamoyo na kila mara
anashughulika na watoto wake Nuru na Matona katika karakana yake ya magari.
Pamoja na hayo, Kizito ana watoto wengine wengi aliozaa na wake zake watatu,
Farida, Mwanaidi na Vingawaje, aliyefariki hivi karibuni.
Mhalifu wa mjini ni Masharubu, tajiri mwenye nguvu
anayemiliki mabanda na biashara za kitapeli. Baada ya kuvumilia matusi kwa muda
mrefu, mkewe alimkimbia na kumwachia binti yao mrembo, Nusura. Nusura ni ua la
yungiyungi lililochanua kwenye lile gheto. Ni mjanja, mwanamke shupavu ambaye
udhaifu wake ni mahusiano yake na Duma, mmoja wa wapangaji wa Masharubu. Duma
ana moyo wa dhahabu lakini anahangaika kimaisha kama DJ mjini Bagamoyo.Karibuni
tu alimleta mdogo wake, Stephen, toka kijijini, ili mvulana huyo aingie shule
ya kujitegemea na kupata fursa ya maisha bora lakini, mpaka muda huu Duma
anashindwa kumtimizia mahitaji muhimu. Muhimu zaidi, Duma anashindwa kuwa mfano
bora kwa mdogo wake, Stephen anayechoshwa na shule na kutaka kuwa ‘mtoto wa
mjini’ kama kaka yake.
Nyendo za Nusura na Kizito zinapishana kuashiria bahati kwa
Kizito, ambaye yuko tayari kuendelea mbele na maisha yake kufuatia kifo cha
mkewe mdogo. Nusura kwa upande wake amechoshwa na wasiwasi katika mahusiano
yake na Duma, hivyo yuko tayari kwa mambo ya kiungwana zaidi. Nusura anajikuta
yuko njia panda kati ya penzi la Duma na lile lililotulia kama maji lenye
uelekeo wa ndoa na Kizito. Hana ufahamu wowote kuwa kuna dhoruba inayochemka
katika maji yale ya samawati. Siri zitasimuliwa, maisha kuchanwachanwa na mioyo
kuvunjwa kwenye mji huu wa Bagamoyo.
Mapitio: (Review)
Tamthilia ya Siri ya Mtungi ni nzuri inayofaa kutazamwa na familia nzima, japokuwa kuna vipande vichache ambavyo si vizuri sana kwa watoto, Tamthilia hii imepangwa vema na mtiririko wenye kueleweka japokuwa nayo ina matatizo kidogo haswa kwa baadhi ya Waigizaji kuongea kama wamekariri, mfano hai ni Mzee Kizito, Stephen na baadhi ya waigizaji...!
Tamthilia ya Siri ya Mtungi ni nzuri inayofaa kutazamwa na familia nzima, japokuwa kuna vipande vichache ambavyo si vizuri sana kwa watoto, Tamthilia hii imepangwa vema na mtiririko wenye kueleweka japokuwa nayo ina matatizo kidogo haswa kwa baadhi ya Waigizaji kuongea kama wamekariri, mfano hai ni Mzee Kizito, Stephen na baadhi ya waigizaji...!
Pongezi kubwa kwa Tamthilia hii, haswa kwa maamuzi yao ya kutumia
mazingira halisi ya Mtanzania wa kawaida na wahusika kuvaa uhalisia...! Muziki wa ala upo kwenye maadhi ya Kitanzania na
nyimbo ni za Kitanzania kwa asiliamia kubwa. Kwa kweli wamejitahidi sana,ukilinganisha
na watayarishaji wengine wa Bongo movies, labda kwa kuwa wanapata surpot na
wataalam kutoka Marekani, na watayarishaji wenye uzoefu wa muda mrefu.
Kuanzishwa kwa tamthilia hii, inaweza kuwa chachu kwa
watayarishaji wengine kuiga yale mazuri, na haswa aina ya upigaji picha,
mazingira na matumizi ya rasilimali za Kitanzania.
Angalia mtitiriko mzima wa tamthilia hii hapa: <<link>>
No comments:
Post a Comment