·
Milioni Kumi Zachakachuliwa.
·
Waandishi Wa Habari Wabebeshwa Lawama.
·
Viongozi Watakiwa Kuachia Madaraka.
Na Iddy
A Ninga
Sakata kubwa limezuka ndani ya mkoa wa Arusha kufuatia wasanii wa filamu
kuhoji juu ya uhalali wa viongozi waliopo madarakani kushikilia nyadhifa hizo.
Hayo yalizuka siku ya jana tarehe saba kufuati kikao
kilichokaliwa na wasanii katika mkoa huo na kusababisha kuzuka kwa malumbano
ambayo yalitaka kusababisha kikao hicho kuvunjika. Katika kikao hicho ambacho
mwanzo kilianza kwa kutaja ajenda sita za kikao hicho na badala yake
ikajadiliwa ajenda moja na kabla ya ajenda haijaisha yalizuka madai ya wasanii
kuhoji juu ya uhalili wa viongozi wa shirikisho la mkoa ambao viongozi hao hao
ndio viongozi wa Arusha movie.
Katika madai ya wasanii hao, walidai kuwa Arusha Movie
imetumia shilingi milioni kumi zilizotolewa na NSSF na vingozi
walipoulizwa kuhusu hilo walidai kuwa pesa hizo zilitolewa kwa ajili ya Arusha
movie na wala siyo kwa ajili ya shirikisho la wasanii wa filamu mkoa wa Arusha.
Akijibu tuhuma hizo Bwana Kasimu Digega ambae ni
mwenyekiti wa wasanii Arusha alisema kwamba wakati pesa hizo zikitolewa yeye
alikuwa mjumbe wa Arusha movie na wala hakua kiongozi bali pesa hizo
zilichukuliwa na viongozi wawili ambao ni Bwana Isack Chalo na Hussen
Sichonge maarufu kwa jina la Ngwasuma.
Hussen Sichonge alikiri kuwa yeye ndie aliehusika na kuchukua pea
hizo na pia alidai kuwa kuna watu wametumwa kuja kuharibu kikao kilichofanyika
siku ya jana. Bwana Hussein Sichonge alianza kutoa lawama zake kwa mwanadada
ajulikanae kwa jina la Neshika kuwa ni mmoja kati ya watu
walo tumwa kuja kuharibu kikao hicho, pia msanii na mwandishi wa habari
ajulikanae kwa jina la Severinus Mwijage alilaumiwa na
bwana Sichonge kuwa na yeye katumwa na Mr Eliasi Magesa ili kuja
kuharibu mkutano huo wa wasanii.
Wasanii hao waliwataka viongozi wa shirikisho kujiuzulu
kufuatia vingozi hao kushikilia nyadhifa mbili tofauti na wasanii kuona kuwa
maslahi yao yanapigwa panga na viongozi wao kwani linapokuja suala la pesa
linabebwa na Arusha Movie na siyo shirikisho.
Wasanii hao waliendelea kudai kuwa muda wa viongo waliopo
madarakani muda wao umeisha na hawatakiwa kufanya tena kazi za shirikisho
kutokana na muda wao kuisha.
Pia bwana Kasimu Digega aliwalaumu waandishi
wa habari wa Arusha kwa kutaka pesa ili kutoa habari za wasanii wa filamu. Hadi
muda huu wasanii wa Arusha wanamsubiri kwa hamu raisi wa Taff Bwana Simon Mwakifamba ili kuja kutoa
suluhisho la jambo hilo na asilimia kubwa ya wasanii wa Arusha wanaonekana
kuukataa uongozi uliopo sasa na kutaka, uongozi mpya ambao utasimama kama
shirikisho na siyo Arusha Movie ambao ni kikundi cha watu wachache.
Kufuatia sakata hilo NSSF wanawajibu wa kutoa kauli juu
ya milioni kumi walizotoa na kufanya semina wasanii wa Arusha huku asilimia
kubwa wakiwa wamejiunga na NSSF.
Hadi sasa bado wasanii wa Arusha hawapo katika muelekeo mzuri
na bado hawaitambui tofauti ya Arusha Movie na shirikisho.
No comments:
Post a Comment