·
Story: Mtitu G. Game
·
Script: Ali M. Yakuti
·
Make-up & Continuity: Mayasa
Mrisho,
·
Camera: Leonard Muhumbira
·
Sound: Rahim Khatibu
·
Editor: Leornard Muhumbira
·
Music: Beny Chaila
·
Mastering: Mtitu G. Game
·
Production Manager: Mayasa Mrisho
·
Assistant Producer: Mayasa Mrisho
·
Executive Producer: Mtitu G Game
·
Director: Mtitu G Game
·
Cast: Jacob Stephen, Rose Ndauka,
Hemed Suleiman, Warda Walid, Patcho Mwamba
Ø Mchambuzi: Iddy A Ninga
The Lost
Adam ni moja kati ya filamu ambayo ningependa kuizungumzia kwa siku ya leo.
Nianzie na
upande wa umri, kwa kifupi filamu hiyo ilikuwa inatakiwa kutazamwa na watu wa
kuanzia umri wa miaka kumi na nane kutokana na kipande ambacho kinamuonyesha
Adamu na Tamara wakiwa wamelaliana juu ya kochi na hiyo ni baada ya mke wa
adamu kuaga anakwenda safari.
Kutokana na
kipande hicho kuwa ni nyeti zaidi na kinaweza kuleta madhara fulani kwa jamii
hasa watoto wadogo ambao umri wao haulingani na kutazama matukio kama kulingana
na umri wao.
Katika
filamu nyingi za kitanzania, wachezaji wengi hasa wa upande wa ulinzi wamekuwa
na mtindo wa kucheza watu wa vituko kitu ambacho katika maisha ya uhalisia
hakipo, na tumeona sasa hivi walinzi ni watu wa kawaida na heshima zao.
Katika
filamu hii mlinzi alikuwa ni mtu wa vituko, jambo kama hili siyo lazima
lionekana sana katika movie zetu kwani kuna uwezekano mkubwa wa kumtoa mtu
katika maisha ya uhalisia.
Kwa upande
wa rangi kuna sehemu rangi za chumba zilikuwa zikiingiliana, mfano tazama
kipande ambacho mke wa adamu alipokea simu ya mume wake. Sauti nayo ilikuwa
inasikika katika hali ambayo haikuwa vizuri sana ingawa ilikuwa ikisikika
vizuri kabisa. Sauti ilikuwa ikisikika kama mtu yupo ndani na muda huo huo mtu
anaonekana yupo nje.
Kwa upande
wa ubunifu, filamu ilikuwa na ubunifu mwingi na kumfanya mtazamaji kujisikia
raha hasa pale ilipogundulika kuwa mke wa Adanu hakufa ila alijichimbia mahali
ili kilinda maisha yake. Pia ubunifu katika familia ya Adamu ulikuwa mzuri na
kusikitisha sana, hasa pale unapotazama jinsi familia ilivokuwa katika hali
fulani ya utofauti wa maisha.
Filamu
ilikuwa nzuri sana ila kwa ushauri wangu, kama filamu ingekuwa na sehemu wa
kwanza peke yake ingekuwa nzuri zaidi na ingekubalika na wengi kwani ukweli ni
kwamba watanzania wengi wanachukia filamu yenye part one na kuendelea...
No comments:
Post a Comment