Thursday 6 February 2014

NIIANGALIAPO TASNIA YA FILAMU YA TANZANIA KWA JICHO LA TATU.




Na.Mwanaidi Mohamed

Binafsi uwa napata tabu sana ninapoangalia filamu za Kitanzania au kwa jina maarufu Bongo Muvi.
Napata tabu za kifikra na mawazo kwa kila sekunde ninayoipoteza kwenye uangaliaji huo.

Wema Sepetu.

Na cha kufurahisha zaidi kila msanii mwenye ofisi basi yeye ni muongozi,muandaaji wa filamu,wakati mwengine yeye ni muhusika mkuu katika muvi hiyo huku yeye ni muongozaji,yeye muandaaji,mhariri,yaani yeye mambo yote yake katika filamu moja,sasa huwa najiuliza mtu mmoja anawezeje kufanya kazi zote hizo.


Sinema za kibongo zimekuwa hazina mvuto hasa kwa kitendo cha kuwaona wachezaji hao hao kila siku,ninaomba kuuliza kwani waigizaji ndio hao hao tu,na kuna baadhi yao katu hutakaa ukamuona anatapangwa katika sehemu za kimasikini kila siku yeye tajiri na hata kama akianzia kwenye umasikini basi mwisho yeye ni tajiri mkuu.

                                                                    
                                                                                         Vicent Kigosi(Ray)
kiukweli sinema za kibongo hazina mvuto kabisa,simshangai mtu aliyepiga marufuku nyumbani kwake kuonyeshwa sinema hizi,zilizojaa mitindo,uhalisia na  tamaduni zisizokuwa za kitanzania.Ninakumbuka niliwahi kuangali movie moja jambazi ameingia katika nyumba kufanya uhalifu kufika mlangoni akavua viatu,hivi kweli jamabazi anaweza kuvua viatu ili afanye uhalifu?nyengine ilikuwa ya marehemu Kanumba jina silikumbuki ila wapo porini huko mtu anapigwa eti marehemu kanumba anacheza ndombolo kweli jamani hili linawezekana?Hii haautaipata sehehmu yoyote isipokuwa katika filamu za kitanzania.

                                                   
                                                       Elizabeth Michael(lulu)
Sababu moja wapo kubwa ni uigizaji kwa ujumla, naweza kukiri kuwa kwa waigizaji wa hapo Bongo, wengi wana vipaji vya uigizaji, lakini kipaji bila ujuzi na ufahamu hauwezi kusaidia kitu, hawa waigizaji wanapaswa kwenda shule za uigizaji ili kunoa na kuvisawazisha vipaji vyao.

Kuna mengi sana katika tasnia hii ambavyo kwa kweli vinatia aibu kwa kiwango kikubwa sana, na haswa linapokuja suala la tafasiri ya Kiingereza, pili mtiririko mzima wa uigizaji wenyewe. Uigizaji wa Bongo muvi umekuwa si wa kuigiza filamu moja na mchezo ukaisha, la hapana. Nilazima kuwepo na sehemu mbili (two Parts). Unapowauliza wanakwambia kuwa wao wapo katika kutafuta pesa na ili filamu ilipe inabidi kuwe na sehemu mbili kikiwezekana mpaka ya tatu. Sawa sikatai lakini basi hizo sehemu moja na mbili kwa nini kuwe na marudio yasiyo na lazima?

Wacha niachane na hayo mambo ya kitaalam, labda nizungumzie swala ambalo linachukuwa sehemu kubwa ya vichwa vya habari za magazeti mengi ya udaku.
Kila kukicha ukitazama kurasa za magazeti (ya Udaku) huwezi kukosa picha za wasanii aidha wa filamu za Bongo muvi au wanamuziki wa Bongo flava. Na habari utakazo zosoma si za kuelimisha jamii hata kidogo,bali ni habari za nani anazini na nani au nani kava nusu uchi na mambo yanayoendana na uharibifu wa jamii.

Leo hii wapo wasanii wanaojiona kuwa wao ni masupasta au wao ni nyota katika tasnia ya filamu za Kitanzania. Lakini je ni kweli wao ni nyota wa kupigiwa mfano, kiasi cha kujiona kuwa wao ndio wao na hakuna wengine zaidi yao?

Hawa wenyewe ujiita Maselebu (celebrities) kwa Kiswahili chepesi tunaweza kusema watu maarufu au Maalum au wenye kujulikana sana.

Lakini tunapokuja kwenye U super star au Nyota wa Sinema, tunaweza kuwaweka katika mafungu kadhaa, aidha ni star katika mchezo (Movie) aloigiza kwa maana ndio alikuwa kiranja au muhusika mkuu, na umaarufu wake unabakia kwenye mchezo huo tu aloucheza na kuna wale ambao u star wao ni kwa kuwa wameweza kuigiza filamu nyingi na katika filamu hizo wameweza kuwa vinara au viranja wa uigizaji, mfano kama vile Manju katika uchezaji ngoma.

Vilevile aweza kuwa ni star kwa kuwavutia watengenezaji filamu maarufu mbalimbali aidha katika nchi au nje ya nchi.
Mtu kama huyu ndio utamkuta kwenye Nyanja za matangazo kwenye runinga au mabango ya matangazo kwenye mabarabara.
Unaweza kuwa superstar tu kama kweli kazi zako zimeweza kukupatia umaarufu wa nje ya mipaka ya nchi yako, kiasi cha kuweza kuhalikwa au kupata zabuni (Tender) ya uigizaji uko nje ya nchi.

Naweza kusema kuwa tunaweza kuwa hatuna Mastaa au masupastaa kwa sababu mbalimbali, lakini sababu moja wapo kubwa ni kwa kukosekana kwa makampuni yenye ushindani wenye kujulikana kuwa hayo makampuni ndio makampuni ambayo yanaongoza katika tasnia ya kutengeneza filamu.

Vilevile tunashindwa kuwa na masupastaa kutokana na mfumo wa nchi wa kutoweza kujuwa viwango vya ulipwaji wa wachezaji filamu, na ili si katika tasnia ya filamu tu, ni tatizo katika njanza zote, kuazia wanasiasa, wafanyabiashara na watu wengine binafsi ambao ni maarufu. Unaweza kusikia mtu anasifiwa kwa majina mbalimbali kama vile pedeshee lakini kazi na biashara anayofanya kiasi cha kutajika jina kwenye muziki haijulikani.

Swala la kuwa selebu (celebrities) kwa maana halisi ya celebrities, ni suala la kuwa na ushawishi katika jamii inayokuzunguka. Hapa sina maana ya ushawishi wa kisiasa tu, hapana. Hata maisha ya kawaida tu kiujumla. Yaani ni mtu ambaye wapenzi wake wapo tayari kumuiga aidha kimavazi au mitindo ya nywele nakadhalika. Vilevile tunategemea selebu huyu awe ni mwenye uwezo wa kipesa na si umaarufu tu wa kuuza sura kwenye runinga. Lakini kwa kibongo bongo unaweza kumuona muigizaji wa filamu za Bongo muvi akijiita maarufu ili hali hana uwezo hata wa kujiendeleza kielimu,au hata kujitibia pale apoumwa.

Lakini kwa Bongo mtu uwa maarufu tu kwa kuwa anatolewa mara kwa mara kwenye magazeti ya Udaku, tena si kwa sifa njema bali kwa sifa ambazo hazina hata maana.
Kwa kweli Napata tabu sana kuweza kujuwa nani ni selebu haswa kwa nchi ya Bongo, hususani kwenye tasnia ya filamu na muziki.

NB:maoni yako ni muhimu kwangu.

No comments:

Post a Comment